17 Oct 2020 / 64 views
Victor Moses atimkia Urusi

Kiungo wa kati wa Chelsea, Victor Moses amekamilisha uhamisho wa mkopo wa msimu mmoja kwenda klabu ya Spartak Moscow ya nchini Urusi baada ya kumaliza mkopo wa Inter Milan.

Spartak imesema kuwa mkopo huo una kipengele cha kumnunua moja moja endapo wataridhika na kiwango cha mchezaji huyo wa kimataifa wa Nigeria.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Nigeria mwenye umri wa miaka 29 aliwahi kucheza kwa mkopo katika klabu ya Fenerbahce ya Uturuki na miamba ya Italia Inter Milan msimu uliopita.

Hajaichezea Chelsea kwa zaidi ya miaka miwili na hii ni mara yake ya sita kutoka Stamford Bridge baada ya kuwasili mnamo 2012.

Uwezekano wa mchezaji huyo kurejea Chelsea ni mdogo sana kutokana na kusajiliwa kwa wachezaji wapya msimu huu na kufanya kupoteza nafasi kwenye kikosi hicho.