16 Oct 2020 / 62 views
Mashabiki kuanza kuingia uwanjani

Mashabiki wa soka nchini Uingereza wanaweza kurejea tena viwanjani hivi karibuni, baada ya ombi la mashabiki kupata saini nyingi kutoka kwenye Bunge la Uingereza ambalo limepanga kuijadili taarifa hiyo Novemba 9, mwaka huu.

Tangu mwezi Machi serikali ilipiga marufuku mashabiki kuingia viwanjani kutokana na ugonjwa wa Corona ulioenea duniani kote na kusababisha matukio mengi kusimama.

Hatua hiyo endapo itafikiwa ni nafuu kwa vilabu vingi ambazo vinategemea zaidi mapato ya mlangoni kuendesha klabu zao.

Licha ya kuchezwa bila ya mashabiki, ligi hiyo imeendelea licha ya ukweli kuwa  imepungua msisimko na ladha, ambapo mpaka sasa zimechezwa raundi nne.

Timu ya Everton inaongoza msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 12 wakishinda mechi zote nne walizoshuka dimbani msimu huu na mechi ijayo ya ligi kuu watacheza dhidi ya Liverpool.