17 Sep 2020 / 70 views
Ivanovic ajiunga na West Bromwich

Klabu ya West Brom imemsaini beki wa zamani wa Chelsea, Branislav Ivanovic kwa mkataba wa mwaka mmoja kuitumikia klabu hiyo.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Serbia mwenye umri wa miaka 36 aliondoka Zenit St Petersburg mnamo Julai baada ya misimu mitatu na nusu nchini Urusi.

Ivanovic alicheza mechi 377 kwa miaka tisa akiwa Chelsea, akishinda Ligi Kuu na Kombe la FA mara tatu, pamoja na Ligi ya Mabingwa na Ligi ya Europa.

Kocha wa West Bromwich amesema "Ameshinda kila kitu katika kazi yake imekuwa nzuri sana. Tumefurahi. Anaongeza ubora na uzoefu uwanjani na nje ya uwanja  katika klabu yetu.

"Kwa hivyo sio yeye tu, ni yeye pamoja na ushawishi atakaokuwa nao sio mabeki tu bali timu nzima inayomzunguka."

Ivanovic alisema: "Ligi Kuu ni ligi bora zaidi ulimwenguni. "Ninahitaji kujipa changamoto na niko tayari kwa changamoto hiyo. Nina furaha kubwa kurudi kucheza kwenye Ligi Kuu."