16 Sep 2020 / 48 views
Reguilon kutua Tottenham

Klabu ya Tottenham wamewasilisha ofa rasmi kwa Real Madrid kumsajili beki Sergio Reguilon ambaye alitakiwa na Manchester United hapo awali.

Manchester United wapo kwenye mazungumzo kwa siku kadhaa, lakini hawapo tayari kulipa Euro Milioni 30 na pia hawapo tayari kukubali Real Madrid kuweka kipengele ambacho kitawapa nafasi ya kumsajili tena Reguilon.
Dili la Reguilon kwenda Spurs bado halijakamilika mbio bado zinaendelea . Spurs wana makubaliano na Real Madrid na sasa wanafanya kazi kukubaliana na mchezaji.

Manchester United walishakubaliana maslahi binafsi na Reguilon siku kadhaa zilizopita , lakini hawana makubaliano na Real Madrid . Spurs wana matumaini ya kumshawishi beki huyo wa kimataifa wa Hispania kuhamia kwao.

Kama Tottenham wakifanikiwa kumsajili Reguilon watakuwa wamekubali vipengele vyote ambavyo Real Madrid wanavitaka. Manchester United hawataki hivyo vipengele kumpoteza mchezaji baadae.