16 Sep 2020 / 63 views
Bale kurejea Tottenham

Klabu ya Tottenham inaendelea na mazungumzo na Real Madrid ili kumsajili tena winga Gareth Bale wakati mchezaji huyo wa kimataifa wa Wales.

Bale, 31, aliondoka Spurs na kujiunga na Real kwa rekodi ya dunia ya uhamisho wa pauni milioni 85 wakati huo 2013 na tangu hapo alifunga zaidi ya mabao 100 na kushinda mataji manne ya Ligi Mabingwa.

Akiwa Spurs, winga huyo alicheza zaidi ya mechi 200 kati ya 2007 na 2013, akifunga mabao 56 na assists 58 na wakala wake amesema kuwa atapenda kumrejesha Bale huko London

Bale amekuwa akihusishwa na Manchester United lakini inaonekana Mashetani Wekundu bado watakosa kumsajili msimu huu wa joto.

Kocha wa Spurs, Jose Mourinho alisema kabla ya mechi yao ya kwanza waliyopoteza kwa bao 1-0 mbele ya Everton Jumapili kwamba alitaka klabu imsajili mshambuliaji kabla ya dirisha la uhamisho kufungwa Oktoba 5.

Huenda makubaliano ya mkopo yakafikiwa lakini TATIZO ni mshahara wa nyota huyo wa Wales kwani anapokea karibu Pauni 600,000 kwa wiki [Bilioni 1.8].