16 Sep 2020 / 55 views
Aubameyang asaini mkataba mpya

Mshambuliaji wa Arsenal, Pierre Emerick Aubameyang ameongeza dili la kuitumikia timu hiyo kwa muda wa miaka mitatu kuitumikia timu hiyo.

Nyota huyo alikuwa kwenye mvutano na mabosi wake wa timu hiyo ambapo awali ilielezwa kuwa alikuwa anahitaji kuondoka ndani ya timu hiyo ili kupata changamoto mpya.

Aubameyang mwenye miaka 31 atakuwa ndani ya Arsenal mpaka mwaka 2023 baada ya kusaini dili hilo ambalo litamfanya awe anavuta mkwanja wa Pauni 250,000 kwa wiki.

Aubameyang amesema:"Mwisho wa siku nimesaini bonge moja ya saini, nina furaha kuwa ndani ya Arsenal.  Hapa ni nyumbani na ni furaha kwangu.

Siku ya leo ni kubwa kwangu na ninahitaji kuwa Legend ndani ya Arsenal na nitakapoondoka niache alama. Ni muda wangu wa kazi na nitapambana.