16 Sep 2020 / 156 views
Tetesi za usajili barani Ulaya

Tottenham huenda wakamtumia kiungo wa kati wa England Dele Alli, 24, chambo wakati wakijaribu kumrejesha Gareth Bale, 31, kutoka Real Madrid.

Everton huenda wakakubali ofa kwa ajili ya wachezaji kadhaa, akiwemo winga wa England Theo Walcott, 31, winga wa Nigeria Alex Iwobi, 24, na mshambuliaji Muitaliano Moise Kean, 20, wakati wakitarajia kuongezea nguvu kikosi cha Carlo Ancelotti.

Mkataba wa miaka mitatu wa mshambuliaji wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang kuichezea Arsenal una thamani ya pauni milioni 55 yakiwemo marupurupu.

Arsenal bado wanapanga kuwaongeza wachezaji zaidi kwenye kikosi chao, huku wakiwalenga kiungo wa kati wa Atletico Madrid Thomas Partey, 27 na kiungo mchezeshaji wa Lyon, Mfaransa Houssem Aouar,22, miongoni mwa wachezaji wanaowataka.

Bayern Munich wako tayari kurudisha shauku yao kwa ajili ya winga Callum Hudson-Odoi, 19, huku wababe hao wa ligi ya mabingwa Ulaya wakiwa na matumaini kuwa Chelsea itapokea ofa yao.

Barcelona itajaribu kumsajili mchezaji wa nafasi ya ulinzi anayekipiga Manchester City Eric Garcia,19, msimu huu ikiwa wataweza kuwauza walinzi wa kati Samuel Umtiti,26, na Jean-Clair Todibo,20. 

Juventus wanakumbana na wakati mgumu kuhusu kumsajili mshambuliaji wa Barcelona Luis Suarez, ambaye anapata changamoto kupata pasi ya Italia kwa haraka.

Inter Milan bado wanamshawishi kumpa mkataba wa kudumu beki wa Chelsea Emerson Palmieri,26. lakini West Ham pia inamtolea macho wakitaka akichezee kikosi hicho kwa mkopo.

Kushindwa kwa Roma kukubaliana Manchester United kuhusu ada ili kumpata beki wa kati Chris Smalling kutaifanya klabu hiyo ya italia kufikiria kuhusu mbadala.

Klabu hiyo inaaminika kutoa ofa ya pauni milioni 3 na marupurupu mengine lakini washika bunduki wanataka dili ya karibu pauni milioni 15 kwa ajili ya mchezaji huyo mwenye miaka 19, ambaye amechezea vikosi vya vijana vya Marekani na England.