16 Sep 2020 / 65 views
Grealish asaini mkataba mpya

Nahodha wa Aston Villa Jack Grealish amesaini mkata mpya wa miaka mitano wa kuendelea kuitumikia klabu hiyo mpaka msimu wa mwaka 2025.

Kiungo huyo raia wa England mwenye umri wa miaka 25 amesaini mkataba mpya hii leo ambao utamfanya aendele kusalia katika klabu hiyo kwa miaka mitano zaidi. Mkataba huo utamfanya kiungo huyo kulipwa mshahara wa pauni laki moja na arobaini (140000) kwa wiki kutoka ule aliokuwa analipwa awali ambao ulikuwa ni pauni Elfu sabini (70000).

 Grealish amekuwa akihusiswa kujiunga na klabu ya Manchester United katika dirisha hili la usajili la majira ya kiangazi ambalo lipo wazi mpaka Oktober 05, lakini klabu ya Aston Villa imempa thamani ya fedha za Uingereza pauni milion 80 kama ada ya uhamisho kiasi ambacho Manchester United hawapo tayari kulipa.

 Mtendaji mkuu wa Villa Christian Purslow amesema wanafaraha kwa Jack kuongeza mkataba na sasa wanaijenga timu hiyo kumzunguka kiungo huyo. Msimu uliopita katika michezo ya ligi kuu alifunga mabao nane na alitoa pasi za usaidizi wa mabao yani assists sita kwenye michezo 36 ya EPL.

 Jack Grealish alijiunga na Aston Villa akiwa na Umri wa miaka nane, na msimu wa 2013-14 alipandishwa kwenye kikosi cha kwanza na mapaka sasa ameshacheza jumla ya michezo 186 na amefunga mabao 25.