01 Aug 2020 / 253 views
Tetesi za usajili barani Ulaya

Uhamisho unaokisiwa wa Jadon Sancho kwenda Manchester United uko karibuni kufikiwa, wakati Borussia Dortmund wakiwa tayari kukubali ada ya awali ya pauni milioni 60 kwa ajili ya winga huyo.

Mshambuliaji wa Mexico Raul Jimenez, 29, yuko njiani kuelekea Manchester United baada ya Wolves kukubali ada ya pauni milioni 27 kumsajili mshambuliaji wa Braga, Mreno Paulinho.

Gareth Bale, 31, amemwambia kocha wa Wales Ryan Giggs kuwa ana dhamira ya kusalia Real Madrid msimu ujao. hata kama kukosa michezo kutaathiri kipato chake.

Chelsea na Manchester City ni miongoni mwa vilabu vinavyoongoza ambavyo vinafuatilia kama mchezaji David Alaba, 28, atasaini mkataba mpya na Bayern Munich.

Leeds wanapanga kusajili wachezaji wawili- Kiungo wa Everton Fabian Delph, 30, na beki Danny Rose,30, wakati huu ambapo kocha Marcelo Bielsa akitafuta wachezaji wenye uzoefu na ligi ya primia. 

Mlinda mlango Muajentina Sergio Romero,33, anataka kufanya mazungumzo na Manchester United kuhusu mustakabali wake- huku Dean Hanserson,23, akirejea Old Trafford baada ya kukipiga kwa mkopo Sheffield United.

Inter Milan wanatarajiwa kukubali dili kumsajili Mshambuliaji Alexis Sanchez,31 kutoka Manchester United kwa mkataba wa kudumu msimu huu. (Manchester Evening News)

Southampton bado wanaisubiri Tottenham kuhusu uhamisho wa kiungo wa kati Pierre-Emile Hojbjerg. Liverpool wanajiandaa kumsajili mchezaji wa Bournemouth Lloyd Kelly, 21, baada ya kupoteza fursa hiyo miezi 12 iliyopita alipokuwa akiichezea timu ya Bristol City.

Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp pia atafanya maamuzi kuhusu mshambuliaji wa Kiingereza Rhian Brewster baada ya mchakato wa kucheza kwa mkopo Swansea kufanikiwa. 

West Ham United wana mpango na mchezaji wa Queens Park Rangers, Ryan Manning, 24. Atletico Madrid imekataa ofa ya pauni milioni 22.6, na kiungo wa kati Matteo Guendouzi, kutoka Arsenal kwa ajili ya kiungo wa kati Thomas Partey.