01 Aug 2020 / 240 views
Liverpool kuimarisha safu ya ulinzi

Klabu ya Liverpool imefanya mawasiliano na Schalke 04 kuhusu upatikanaji wa beki wao wa kati Ozan Kabak ili kuimarisha eneo la beki ambalo limeonekana kuyumba msimu huu.

Jurgen Klopp ni shabiki mkubwa wa beki huyo wa kati ambaye anahitaji Anfield kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Dejan Lovren ambaye amehamia klabua ya Zenit St. Petersburg ya nchini Urusi

Schalke wanahitaji hela na Kabak kwenye mkataba wake kuna kipengele ambacho kinaeleza anaweza kuuzwa kwa pauni milioni 41 majira yajayo ya kiangazi mwaka 2021.

Liverpool wanaweza kufanya biashara ya kumpata kwa chini ya hapo majira haya ya kiangazi kutokana na uhitaji wa fedha wa Schalke kwa kipindi kutokana na janga la Corona.

Kabak ni miongoni mwa safu bora ya Uturuki pamoja na Caglar Soyuncu wa Leicester na Merih Demiral wa Juventus hivyo Liverpool wamaweza kuimarisha safu yao ya beki kama watafanikiwa kupata saini ya beki huyo.