01 Aug 2020 / 43 views
Zaha ataka kuondoka Crystal Palace

Kocha wa Crystal Palace, Roy Hodgson amesema kuwa mchezaji wa timu hiyo, Wilfred Zaha yupo tayari kuondoka ndani ya klabu hiyo msimu huu.

Winga huyo wa kimataifa wa Ivory Coast mwenye umri wa miaka 27 alihusishwa na kutakiwa na Everton na Arsenal msimu uliopita lakini mpango huo haukufaulu na Hodgson anasema uvumi huo uliathiri uwezo wa mchezaji msimu huu.

"Ni wazi ilimuathiri kwa sababu fomu yake katika wiki chache zilizopita imekuwa duni kabisa""Ni shida kwa klabu na shida kwake ikiwa ameamua kuondoka. Ikiwa anahisi hataki kuwa na sisi tena, hiyo inaweza kuwa ya kusikitisha.

"Bado tunampenda sana; hatuwezi kumfanya kama sisi. Hii ni hali ambayo yeye na klabu wanaweza kusuluhisha. Sina jibu."

Zaha, alikuzwa na Academy ya Palace na aliondoka kujiunga na Manchester United mnamo 2013 kabla ya kurudi tena viunga vya Selhurst Park mnamo 2014, awali ilikuwa kwa mkopo.

Anajulikana kwa ujanja wake, mbio na Chenga, Zaha alifunga mabao 10 ya ligi mnamo 2018-19 lakini alifanikiwa kufunga magoli Manne tu msimu huu, idadi ndogo kabisa ya kazi yake tangu msimu wa 2015-16.