30 Jul 2020 / 44 views
Liverpool yapanda kithamani

Klabu ya Liverpool inaikaribia timu ya Manchester United kuwa klabu yenye thamani kubwa zaidi England baada ya kutwaa taji la Premier League hii ni kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa Brand Finance Football Annual.

Majogoo hao wa England sasa wakiwa nafasi ya nne Duniani na thamani yao imeongezeka kwa asilimia sita hadi kufikia paundi bilioni 1.143 (€1.262bn), wakiwa nyuma ya Manchester United kwa paundi milioni 47.

United wenyewe kwa sasa wana thamani ya paundi bilioni 1.190 wakishuka kwa paundi milioni 143 ambapo kwa sasa wanashika nafasi ya tatu katika thamani ya Vilabu duniani.

Hata hivyo klabu hizo mbili bado zipo nyuma ya miamba ya soka ya LaLiga, Real Madrid ikiongoza na Barcelona ikiwa katika nafasi ya pili.

KLABU 10 ZENYE THAMANI KUBWA ZAIDI DUNIANI.

1. REAL MADRID £1.286bn / 13.8 per cent- (£205m Imeshuka)

2. BARCELONA £1.280bn / 1.4 per cent + (£18.1m Imepanda)

3. MANCHESTER UNITED £1.190bn / 10.7 per cent – (£143m Imeshuka)

4. LIVERPOOL £1.143bn / 6 per cent + (£64.3m Imepanda)

5. MANCHESTER CITY £1.018bn / 10.4 per cent – (£118m Imeshuka)

6. BAYERN MUNICH £957m / 19.6 per cent – (£233m Imeshuka)

7. PSG £876m / 5.8 per cent + (£48m Imepanda)

8. CHELSEA £859m / 1.9 per cent – (£17m Imeshuka)

9. TOTTENHAM HOTSPUR £710m / 3.3 per cent + (£23.5m Imepanda)

10. ARSENAL £651m / 18.18 per cent – (£150m Imeshuka)