30 Jul 2020 / 50 views
Messi kubakia Barcelona

Mshambuliaji wa Barcelona, Lionel Messi amebakiza mwaka mmoja tu kwenye mkataba wake wa kuendelea kuwatumikia Barcelona na anaonekana kutokuwa na furaha ndani ya miamba hiyo ya Cataluna aliyoitumikia kwa miaka yake yote.

Barcelona wamepoteza taji la la liga na wanapitia kipindi kigumu, hali inayodaiwa kutokumfurahisha Lionel Messi.

Kumekuwepo na taarifa kwamba hali hiyo imemfanya Messi atamani kutimka Barcelona na kujaribu changamoto mpya sehemu nyingine. Baba yake Messi ambaye pia ni walala wake amehamishia baadhi ya biashara zake Milan, hali iliyochagiza zaidi kuwa huenda yupo katika mazungumzo na club ya Inter Millan juu ya uhamisho wa Messi.

Taharuki ilizidi zaidi siku ya Jumanne ambapo Messi alionekana mjini Milan. Ila Marrota amesema hawahusiani na uwepo wa Messi Italia, ni taarifa za uzushi tu. Alisema kiongozi huyo wa Inter Millan.

Marrota alisema "Hizi ni taarifa tu, ila hazituhusu. Kila timu inatamani kuwa na Lionel Messi. Ila kwa hali ilivo sasa hivi, hakuna timu yoyote ya Italy itakayoweza kumsajili Lionel Messi."