30 Jul 2020 / 56 views
Chilwell kutua Chelsea

Kocha wa Tottenham Hotspur Jose Mourinho anataka kumsajili winga anayekipiga Porto, raia wa Colombia Luis Diaz.

Inter Miami, inayomilikiwa na nahodha wa zamani wa England David Beckham, ina mpango wa kumfanya mshambuliaji wa Barcelona Luiz Suarez kuwa chaguo lao la kwanza kubwa la usajili

Wakala wa mchezaji anayetolewa macho na Manchester City na Paris St-Germain David Alaba, ameitaka Bayern Munich kumlipa mchezaji beki huyo wa kushoto, 28, pauni milioni 18 kuongeza mkataba wake.

Mazungumzo kati ya Manchester United na mlinda mlango wa Kiingereza Dean Henderson, 23- ambaye ametumia msimu wake akichezea Sheffield United kwa mkopo- yamekuwa kwenye hatua muhimu baada ya kufanyika kwa majuma kadhaa.

Atletico Madrid imekataa ofa ya pauni milioni 22.6, na kiungo wa kati Matteo Guendouzi, kutoka Arsenal kwa ajili ya kiungo wa kati Thomas Partey,

Chelsea imeweka kipaumbele katika kumsajili beki wa kushoto wa Leicester City Ben Chilwell, 23, miongoni mwa machaguo mengine ya nafasi hiyo, akiwemo mchezaji wa nafasi ya ulinzi wa Ajax Muajentina Nicholas Tagliafico.

Watford iko kwenye mazungumzo na Vladimir Ivic kuhusu nafasi ya kocha iliyo wazi baada ya Mserbia huyo, 43 kuondoka Maccabi Tel Aviv, ambako alinyakua mataji kadhaa ya ligi, mfululizo.

Mshambuliaji Mbrazili Hulk, 34, anafikiria kuhamia ligi ya primia mkataba wake na Shanghai SIPG utakapokwisha mwezi Januari.

Leeds United wanamuwinda beki wa kulia wa FC Utrecht, Sean Klaiber. Hata hivyo matumaini ya Leeds ya kumsajili winga Thiago Almada yanafifia, huku mchezaji huyo, 19 akiwaambia wachezaji wenzake wa timu ya Velez Sarsfield kuwa anataka kubaki katika ardhi ya nyumbani kwake

Mlinda mlango wa zamani wa Burnely, West Ham na Manchester City Joe Hart, karibuni kujiunga na mabingwa wa ligi ya Uskoti, Celtic.

Barcelona wanatarajia kumuuza Martin Braithwaite, 29. Mshambuliaji huyo si mchezaji aliye kwenye mipango ya kocha Quique Setien msimu ujao.