30 Jul 2020 / 46 views
Willian kuwaniwa na vilabu vikubwa

Timu tano zinamuwania Kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil na klabu ya Chelsea ya Uingereza Willian kwa mujibu wa wakala wa mchezaji huyo Kia Joorabchian.

Miongoni mwa vilabu hivyo viwili ni vya ligi kuu England EPL, nyingine ni kutoka ligi ya soka Marekani MLS.

Mkataba wa Willian ndani ya Chelsea unamalizika mwishoni mwa msimu huu na klabu ya Chelsea ilimpa ofa ya kumuongeza mwaka mmoja lakini mshambuliaji huyo anataka mkataba wa miaka 3.

 Agosti 9 mwaka huu Willian atatimiza miaka 32 hivyo kwa mujibu wa sera za Chelsea mchezaji huyo ni ngumu kupewa mkataba wa zaidi ya mwaka mmoja ingawa Kocha wa kikosi hicho Frank Lampard amenukuliwa akisema anamuhitaji Mbrazil huyo msimu ujao, 

Klabu za Tottenham, Arsenal na Manchester United za England zinatajwa kuiwania saini ya Willian na Inter Miami inayomilikiwa na mchezaji wa zamani wa Manchester utd na Real Madrid Mwingereza David Beckam inayoshiriki ligi kuu ya Marekani MLS.

 Wakala wa mchezaji huyo Kia Joorabchian amesema Willian bado hajafanya maauzi ya kusalia Chelsea lakini anataka amalize kwa msimu ndipo atakapo fanya maamuzi juu ya wapi anaelekea,

Baada ya ligi kuu England kumalizika Chelsea imesalia na mchezo wa Fainali ya kombe la FA dhidi ya Arsenal utakaochezwa August 1, na michuano ya klabu bingwa barani ulaya UEFA Champions League ambapo wataminyana na Bayern Munic katika mchezo wa marudiano hatua ya 16 bora.