30 Jul 2020 / 51 views
Oscar ataka kucheza taifa la China

Kiungo mshambuliaji wa Brazil Oscar anataka kuichezea timu ya taifa ya China endapo FIFA watamruhusu licha ya kanuni ngumu za FIFA kwa mchezaji aliyokwisha kuchezea mechi rasmi ya Timu ya Taifa kwa wakubwa.

Oscar aling'ara sana akiwa na timu ya Chelsea ya England ambayo aliitumikia kwa miaka  4 tangu mwaka  2012-2016 na baadaye kutimukia China kwenye timu ya Shanghai SIPG anayoichezea hadi sasa.

Kutimkia kwake China kulipelekea asiitwe  tena  katika timu ya Taifa ya Brazil aliyoichezea  michezo 47 na kuifungia magoli 12 na mechi yake ya mwisho ilikuwa mwaka 2015 dhidi ya  Peru katika mchezo wa kuwania kufuzu kombe la dunia 2018

Timu ya Taifa ya China imeonesha nia ya kumuhitaji kiungo huyu mshambuliaji ambaye anang'ara katika ligi hiyo japo tatizo ni hizo kanuni za FIFA.