30 Jun 2020 / 24 views
Dean Henderson kubakia Sheffield United

Kipa wa Sheffield United, Dean Henderson amekubali kuongeza mkataba wake wa mkopo kutoka Manchester United kubakia Sheffield United hadi mwisho wa msimu.

Alitakiwa kurudi Old Trafford mnamo Juni 30, lakini ameruhusiwa kubaki huko Bramall Lane kwa mechi zao saba za mwisho za ligi.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 amekuwa katika fomu nzuri kwa The Blades msimu wa sasa, akiwa na clean sheets 11 ndani ya Premier League na kuisaidia klabu yake kushika nafasi ya nane kwenye msimamo wa PL.

Pamoja na Henderson, Sheffield United wamewaongeza mikataba mabeki, Phil Jagielka na Kieron Freeman na kiungo, Jack Rodwell na mshambuliaji, Leon Clarke kwa kipindi chote cha msimu huu.

Lakini kiungo Mo Besic amerejea Everton na beki, Panos Retsos amerejea Bayer Leverkusen baada ya mikopo yao kumarizika ndani ya klabu hiyo.