30 Jun 2020 / 23 views
Matip kukaa benchi mpaka mwisho wa msimu

Beki wa Liverpool, Joel Matip atakosa mechi zilizobaki za msimu kutokana na jeraha la mguu alilopata mchezaji huyo wa kimataifa wa Cameroon.

Beki huyo wa Liverpool Matip, ambaye amecheza michezo 13 katika mashindano yote msimu huu, alipata jeraha hilo wakati mechi ya ligi dhidi ya Everton.

Pia Matip alikosa mechi ambapo Liverpool walishinda 4-0 dhidi ya Crystal Palace wiki iliyopita na kuendelea kuongoza ligi hiyo mpaka kushinda taji hilo.

"Msimu huu sitarudi kwenye uwanja lakini kwa msimu ujao, natumai nitakuwa msaada wa moja kwa moja kwa timu," Matip aliambia tovuti ya Liverpool.

Matip alikosa siku 84 za hatua za mapema kwenye kampeni kutokana na jeraha la goti kabla ya kupona na kurejea uwanjani na kuendelea na kucheza.