30 Jun 2020 / 108 views
Kurzawa asaini mkataba mpya PSG

Beki wa Paris Saint-Germain, Layvin Kurzawa amesaini mkataba mpya wa miaka minne na mabingwa hao wa Ufaransa mkataba utakaomuweka kwenye klabu hiyo mpaka mwaka 2024.

Mnamo Januari, kulikuwa na uvumi wa yeye kuhamia Arsenal baada ya kubadilisha wakala wake lakini sasa ameamua kubakia ndani ya klabu hiyo na kusaini mkataba mpya.

Kurzawa sasa anawakilishwa na Kia Joorabchian, ambaye alifanya biashara ya kuwaleta David Luiz na Cedric Soares kuhamia viunga hivyo vya Emirates.

Kurzawa amecheza mechi 123 kwa PSG, akifunga mabao 13 ambayo ni pamoja na hat-trick ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Anderlecht mnamo 2017... Ameshinda mataji 14 katika misimu mitano hadi sasa huko Paris.

Baada ya kuanza kazi yake huko Monaco, Kurzawa alijiunga na PSG mnamo 2015 kwa €23 milioni, akisaini mkataba wa miaka mitano na miamba hao wa Ligue 1.