30 Jun 2020 / 26 views
Valencia wamfukuza kocha wao

Klabu ya Valencia wamemfukuza kocha wao Albert Celades kutokana na mwenendo mbovu wa timu kwenye michuano ya La Liga huku mkurugenzi wa michezo wa Klabu hiyo Cesar Sanchez akijiuzulu.

Voro Gonzalez amechukua nafasi ya Celades kama meneja hadi mwisho wa msimu kuingoza klabu hiyo kwa mechi zilizobakia nchini Italia.

Alichukua madaraka mnamo 2008 baada ya Ronald Koeman na kuisaidia timu kutoshuka daraja La Liga.

Celades alichaguliwa kuwa kocha wa Valencia mnamo Septemba mwaka jana baada ya kufukuzwa kwa kocha Marcelino ndani ya klabu hiyo.

Anakuwa kocha wa sita kufukuzwa ndani ya klabu hiyo tangu Bilionea wa Singapore Peter Lim anunue klabu hiyo mwaka 2014, wakati Sanchez - aliyeteuliwa Januari - ndiye mkurugenzi wa sita wa michezo kuondoka katika kipindi hicho hicho.

Sanchez alijiuzulu muda mfupi baada ya kusema kuwa Celade bado atasimamia mchezo wa Jumatano dhidi ya Athletic Bilbao.

Valencia ni ya nane katika msimamo wa La Liga, na wamepoteza michezo yao mitatu kati ya minne iliyopita ya ligi hiyo.