30 Jun 2020 / 28 views
Buffon asaini mkataba mpya Juve

Kipa wa Juventus Gianluigi Buffon ametia saini mkataba mpya wa mwaka mmoja na klabu hiyo utakaomalizika mwaka 2021 na viongozi hao wa Serie A.

Mchezaji huyo wa zamani wa Italia, ambaye atakuwa na umri wa miaka 43 wakati mkataba wake mpya utakapomalizika, alirudi Juventus mnamo 2019 baada ya msimu mmoja huko Paris St-Germain.

Buffon amecheza mechi zaidi ya 500 za ligi kwa Juventus tangu ajiunge na Klabu hiyo mnamo 2001 akitokea klabu ya Parma aliyoanza kucheza mwaka 1995.

Naye Nahodha wa Juve Giorgio Chiellini pia amesaini mkataba mpya wa mwaka mmoja ndani ya klabu hiyo ya Italia.

Juventus wanaongoza ligi kwa alama nne kileleni mwa Serie A na michezo imebakia 10 kumalizika kwa ligi hiyo ambapo Juve anatafuta taji la 10 mfululizo.