
Wolves kumuuza Raul Jimenez
Klabu ya Wolves wameripotiwa kuweka bei yao ya kumuuza Raul Jimenez kuwa ni €100 (Pauni 91m), na mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Mexico Anawindwa na Manchester United msimu huu.
Jarida la Uhispania AS, limeripoti kuwa klabu hiyo ya Molineux inatamani kumbakiza Jimenez licha ya kuongezeka kwa ofa za vilabu kutaka saini yake, licha ya United pia wamo Juventus na Real Madrid kwenye mbio hizo.
Jimenez amekuwa katika kiwango cha juu kwa Wolves msimu huu, akiwa amefunga mabao 14 kwenye Premier League na kwa ujumla ana magoli 23 katika mashindano yote kwa klabu hiyo ya Mreno, Nuno Espirito Santo mwenye asili kutoka visiwa vya Sao Tome.
Pia Arsenal imeripotiwa kuwa haitamsajili Dani Ceballos wakati mkopo wake kutoka Real Madrid utakapomalizika - kwani kiungo huyo hajafanya ya kutosha kumvutia meneja wa The Gunnes, Mikel Arteta.
Ceballos yuko wazi kujiungana na klabu nyingine ya Premier League, akiwa na umri wa miaka 23 hana nia ya kurudi Bernabeu kwani bado haaminiwi kuwa sehemu ya mipango ya kocha wa Madrid, Zinedine Zidane.
Ceballos alifunga goli la ushindi dakika za mwisho Arsenal ikisonga Nusu fainali ya FA Cup dhidi ya Sheffield United Jumapili, na The Gunners walikubaliana na Madrid kuongeza mkopo wake hadi mwisho wa msimu.
Lakini sasa chini ya Arteta hatma yake huko Emirates haina uhakika, tangu aliposainiwa na mtangulizi wa Arteta, Unai Emery kama mbadala wa Aaron Ramsey msimu wa joto uliopita.