30 Jun 2020 / 23 views
Arthur Melo kujiunga na Juventus

Klabu ya Barcelona wamethibitisha kumuza Arthur Melo kwenda Juventus kwa dau la Euro milioni 72, pamoja na malipo ya ziada ya Euro milioni 10 ikiwa baadhi ya malengo yatafikiwa.

Dili hilo limeambatana na mabadilishano ya wachezaji, huku Barca ikionekana kuwa na nia ya kumuuza Arthur kwa ajili ya kumnasa Miralem Pjanic, mwenye miaka 30.

Uhamisho wa Pjanic unatarajiwa kuthibitishwa katika siku zijazo, akitajwa kuwa na dau la uhamisho takribani Euro milioni 60, hivyo Barcelona watapata ziada ya €10m katika dili hilo kusaidia kuweka sawa hesabu kwenye vitabu vyao vya mauzo kwa msimu wa 2019/20.

Barcelona wamethibitisha kwamba Arthur atabaki klabuni hapo kwa muda wote wa msimu huu, na atajiunga na Juventus katika msimu wa 2020/21.

Arthur alijiunga na Barca akitoka Gremio kwa ada ya takribani € 30m mnamo mwaka 2018, na amekuwa kiungo bora huko Camp Nou, akifanikiwa kucheza mechi 72 hadi sasa.