29 Jun 2020 / 32 views
Gomes kuondoka Manchester United

Kiungo mshambuliaji wa Manchester United, Angel Gomes anaweza kuondoka klabuni hapo wakati mkataba wake utakapomalizika mnamo Juni 30.

Mazungumzo juu ya mkataba mpya yamekuwa yakifanyika na Solskjaer alisema wiki iliyopita alikuwa na matarajio mazuri ya makubaliano yatakubaliwa.

Walakini, hakuna maendeleo yoyote na Gomes, 19, mwishoni mwa wiki hivyo uhenda mchezaji huyo akaondoka ndani ya klabu hiyo.

"Sijasikia chochote jana usiku au asubuhi hii," Solskjaer alisema Jumatatu. "Ikiwa hali bado ni hivyo, jibu ni fupi: ndio ataondoka."

Gomes, ambaye amekuwa na United tangu umri wa miaka sita, amcheza ekwa dakika 19 tu kwenye Ligi Kuu msimu huu.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza mwenye umri wa chini ya miaka 20 alikuwa mchezaji wa mapema kabisa wa Ligi Kuu wakati alitoka benchi akiwa na umri wa miaka 16 siku 263 dhidi ya Crystal Palace mnamo Mei 2017.