14 Jan 2020 / 29 views
Rooney aanza kuendesha gari

Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United, Wayne Rooney ameanza kuendesha gari nchini Uingereza baada ya kumaliza kifungo cha miaka miwili cha kutoendesha gari.

Rooney ambaye sasa ni kocha mchezaji wa Derby County inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza Uingereza (Championship), alifungiwa kuendesha gari na mahakama baada ya kupatikana na hatia ya kuendesha akiwa amelewa mwaka 2017.

Rooney mwenye magari mengi ya kifahari ya kila aina, licha ya kujaza ndinga kibao nyumbani kwake, hakuwa na uwezo wa kuendesha gari kwa miaka miwili.

Wenzetu wanazingatia sana sheria ya Drive Under Influence (DUI), yaani kuendesha ukiwa na kiwango kikubwa cha kilevi.

Rooney alionekana akiwa na shauku ya kuendesha alipokuwa akitinga kwenye gari lake la kifahari la Land Rover Overfinch lenye thamani ya pauni 219,000 (Sh milioni 656).

Rooney, 34, inasemekana ametoka Marekani ambako alikuwa akicheza DC United na kutua Derby kwa ushawishi wa mkewe baada ya ndoa yao kuonekana ikisua sua nchini Marekani.