13 Jan 2020 / 54 views
Manchester United kumsajili Fernandez

Klabu ya Manchester United na Sporting Lisbon imeanza mazungumzo juu ya uhamishaji wa Bruno Fernandes kwa Pauni milioni 60.

Kiungo wa kati Fernandes mwenye umri wa miaka 25 alifunga mara mbili wakati Sporting ilipoifunga Vitoria Setubal 3-1 katika mechi iliyofanyika Jumamosi.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno ana hamu ya kusonga mbele lakini hakukuwa na makubaliano kati ya vilabu juu ya ada ya uhamisho.

Meneja wa United Ole Gunnar Solskjaer na msaidizi wake, Mike Phelan, walimtazama mchezaji huyo alipocheza dhidi ya FC Porto mnamo 5 Januari.

Solskjaer amekataa kuzungumza hadharani juu ya Fernandes na amesisitiza kwamba klabu hiyo itasaini malengo ya muda mrefu tu katika dirisha la Januari la kuhamisha, licha ya majeraha kwa wachezaji wa kati Paul Pogba na Scott McTominay.

Manchester United ni ya tano kwenye msimamo wa ligi kuu soka nchini Uingereza alama tano nyuma ya Chelsea iliyopo nafasi ya nne kwenye vita ya kuwania nafasi ya Ligi ya Mabingwa.