03 Dec 2019 / 30 views
Rapinoe ashinda tuzo ya wanawake

Mchezaji wa Marekani, Megan Rapinoe ameshinda tuzo ya Ballon d'Or kwa Wanawake mwaka 2019 baada ya kumshinda Lucy Bronze wa Uingereza.

Rapinoe mwenye umri wa miaka 34 aliisadia Marekani kushinda kombe la dunia mwaka huu nchini Ufaransa ambapo alikuwa mchezaji bora wa mashindano na mfungaji bora bora wa mashindano hayo baada ya kushinda magoli sita.

Bronze alikuwa mchezaji bora wa wanawake wa Ulaya mwaka huu alishiriki michuano ya dunia mwaka huu akiwa na timu ya taifa ya Uingereza.

Kwenye kinyang’anyiro hicho Alex Morgan wa Marekani alishika nafasi ya tatu kutokana na uwezo wake alionesha kwenye michuano ya kombe la dunia.

Mshambuliaji wa Lyon Ada Hegerberg, ambaye alikua mshindi wa kwanza wa tuzo ya wanawake mwaka jana, alimaliza wa nne, wakati mchezaji wa Arsenal na Uholanzi Vivianne Miedema alishika nafasi ya tano.

Rapinoe, ambaye hakuhudhuria sherehe hiyo ya tuzo, alisema kwa ujumbe uliorekodiwa: "Nimesikitisha sana sikuweza kufika usiku wa leo ila nashukuru kwa kushinda tuzo hii’.

Pia aliongeza kusema "Siwezi kuamini kuwa mimi ndiye ninashinda kwenye uwanja huu, imekuwa ni mwaka mzuri. Nataka kuwashukuru wenzangu na shirikisho la Marekani."