03 Dec 2019 / 33 views
Gurdiola bado auwaza ubingwa EPL

Kocha wa Mnchester City, Pep Guardiola amedai bado wana nafasi ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu Uingereza licha ya kuachwa alama 11 na Liverpool.

Liverpool ina pointi 40 kileleni huku Man City wakiwa na pointi 29, katika historia ya Premier hizo ni pointi nyingi zaidi kihistoria baada ya mechi 14, na timu zote mbili ambazo awali zilifikisha pointi hizo ndani ya mechi hizo zilitwaa ubingwa, ambazo ni Tottenham 1961-62 na Man City 2017-18.

Leicester City wamebakiza pointi nane waifikie Liverpool lakini hawaonekani kuwa wapinzani wakubwa wa ubingwa kwenye ligi hiyo.

Liverpool juzi walifanikiwa kuwachapa Brighton mabao 2-1 kwenye mchezo ambao walipata pigo baada ya kipa wao Alisson Becker kupewa kadi nyekundu.

“Tunaonekana kuendelea vizuri, lakini wigo wa pointi kwenye Ligi Kuu England mara nyingi huonyesha tofauti kwenye mchezo wa mwisho, hivyo ni vyema tukasubiri,” alisema kocha wa Liverpool, Juggen Klopp.

Guardiola alipoulizwa kama anaamini sasa vita ya ubingwa imeisha, alisema: “Tuna mpinzani mwingine mbele yetu, sasa tunatakiwa kujaribu kushinda michezo, kushinda michezo na kuona kitakachotokea.

“Nilisema jana kuwa siyo wazo zuri kufikiria kuhusu Premier au kufikiria pointi nyingi ulizoachwa.

Tunatakiwa kushinda michezo, kushinda michezo, na unapokuwa hushindi, itakuwa ngumu zaidi.”