02 Dec 2019 / 127 views
Mancini aipamba Man City mbio za ubingwa

Kocha wa zamani wa Manchester City, Roberto Mancini amekataa kuitoa timu yake hiyo ya zamani kwenye mbio za kuwania ubingwa licha kuwa nyuma kwa alama 11 dhidi ya Liverpool anayeongoza ligi hiyo.

Manchester City ilitoka 2-2 na Newcastle United kwenye mechi ya ligi kuu siku ya Jumamosi na kuiruhusu Liverpool kuongoza ligi hiyo kwa tofauti ya alama 11 baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Brighton.

Vijana hao wa Jurgen Klopp wanaongoza ligi hiyo kwa alama nane dhidi ya Leicester City ambaye alishinda 2-1 dhidi ya Everton kwenye mechi iliyopita.

Licha ya matokeo hayo Mancini ambaye aliiongoza City kupata taji la Ligi Kuu na Kombe la FA wakati utala wake amesema Klabu yake ya zamani haiwezi kutolewa kwenye mbio za ubingwa msimu huu.

"Nadhani Liverpool katika miaka miwili iliyopita ni timu madhubuti Lakini nakumbuka mwaka jana mnamo Novemba na Desemba Manchester City walikuwa nyuma kwa alama saba dhidi ya Liverpool na akashinda kombe Man City” Alisema Mancini.

Ligi kuu soka nchini Ungereza inaendelea tena katikati ya wiki hii huku Manchester City akicheza dhidi ya Burnley na Liverpool akiwa nyumbani akicheza na Evertoon.