02 Dec 2019 / 40 views
Southgate atamani rekodi ya Euro

Kocha wa Uingereza, Gareth Southgate amesema kuwa rekodi ya timu yake kwenye Mashindano ya Ulaya imekuwa nzuri lakini timu hiyo ina nafasi ya kufanya vizuri tena kwenye michuano hiyo mwakani.

Uingereza ambao walimaliza nafasi ya nne kwenye michuano ya kombe la dunia iliyofanyika mwaka 2018 nchini Urusi na wamewahi kufika kweye hatua ya nusu fainali ya mchuano ya Euro mara moja ambapo Southgate alikwa mchezaji wakati huo.

"Fursa ni sisi kwenda mbali zaidi kwenye michuano hiyo hivyo tunaahaidi kufanya vizuri kwenye michuano hiyo itakayofanyika mwakani” Alisema Southage.

"Wanayo nafasi ya kuishawishi nchi yetu tena. Wanajua kile kilichohisi kama miaka miwili iliyopita tulivyofanya vizuri kwenye michuano ya kombe la dunia” Aliongeza Southgate.

Uingereza wamepangwa kundi moja pampja na imu za  Croatia, Jamhuri ya Czech na ama Scotland, Israel, Norway au Serbia katika kundi D ambapo watacheza mechi za mtoaono. Wataanza mechi yao ya kwanza dhidi ya Croatia mnamo 14 Juni mwakan.

Uingereza itacheza michezo yao yote mitatu ya makundi katika uwanja wa Wembley, ambayo pia itakuwa mwenyeji wa mechi za nusu fainali na fainali.