02 Dec 2019 / 39 views
Solskjaer hajali nafasi waliokuwa nayo EPL

Kocha wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer amesema kuwa hajali sana nafasi waliyopo kwenye msiamo wa ligi kuu soka nchini Uingereza.

Kauli ya kocha huyo imekuja baada ya Manchester United kutoka 2-2 dhidi ya Aston Villa kwenye mechi iliyofanyika katika uwanja wa Old Trafford na kubakia nafasi ya tisa kwenye msimamo wa ligi.

Kama Manchester United wangeshinda mechi hiyo wangepanda hadi nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi kuu soka nchini Uingereza lakini wameshindwa kufanya hivyo kwenye mechi hiyo.

"Nisingekuwa nimekaa hapa na kuongea juu yetu kuwa wa tano ikiwa tunapata bao moja la ziada, kwa hivyo msimamo wa ligi katika hatua hii sio wasiwasi mkubwa kwa sababu ni ngumu sana," Solskjaer alisema.

"Tuliunda nafasi nyingi ambazo zinapaswa kushinda mchezo huu lakini kwa ujumla sidhani kama tulistahili, haswa baada ya kipindi cha kwanza."

United ambao hadi sasa wana jumla ya alama 18 baada ya kucheza michezo 14 kwenye ligi kuu soka nchini Uingereza.