02 Dec 2019 / 56 views
Goli la Messi laiangamiza Atletico Madrid

Mshambuliaji wa Barcelona, Lionel Messi ameifungia goli la ushindi klabu yake dakika za mwisho kwenye mechi ya ligi kuu dhidi ya Atletico Madrid.

Messi alifunga goli hilo dakika ya 86 baada ya kubanana vilivyo katika kipindi cha kwanza kwenye mechi hiyo ambayo ilikuwa kali sana kutokana na ubora wa kila timu kwenye ligi hiyo.

Marc-Andre ter Stegen hapo awali alifanya saves mbili nzuri kutoka kwa wachezaji wa Atletico Madrid, Mario Hermoso na Alvaro Morata.

Baada ya ushindi huo Barcelona wamepanda kutoka nafasi ya tatu hadi nafasi ya kwanza akimshusha Real Madrid kwenye msimamo wa La Liga.

Atletico Madrid walikosa nafasi kadhaa za kuongoza kwenye mechi hiyo lakini walishindwa kutokana ubora wa golikipa wa Barcelona, Ter Stegen.

Real Madrid wao ilishinda 2-1 dhidi ya Alaves siku ya Jumamosi huku Sevilla ikishinda 1-0 dhidi ya Leganes na kupata mpaka nafasi ya tatu kwenye msimamo wa La Liga.