16 Nov 2019 / 43 views
Messi awafunga Brazil

Mshambuliaji wa Barcelona, Lionel Messi amefunga bao lake la kwanza kwa Argentina baada ya miezi mitatu kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Brazil nchini Saudi Arabia.

Messi alifunga goli hilo baada ya kukosa penati iliyookolewa na mlinda mlango wa Brazil Alisson Becker wa Liverpool lakini dakika 69 ya mchezo huo akashinda goli na kuwapa ushindi Argentina  kwenye mechi hiyo.

Messi amecheza mechi hiyo baada ya kumaliza adhabu yake ya miezi tatu kutokana na kauli yake kuwa shirikisho la soka America ya kusini walichukua rushwa kwa Brazil ili wawasaidie kushinda kombe la Copa America.

Argentina anatarajia kucheza na Uruguay kwenye mechi ya kirafiki itakayofanyika Tel Aviv Jumatatu lakini mchezo huo unaweza kufutwa kwa sababu ya mapigano huko Israeli.

Brazil itacheza na Korea Kusini huko Abu Dhabi Jumanne mchezo wao wa mwisho kabla ya kucheza mechi za kuwania kufuzu michuano ya Kombe la Dunia la 2022 kuanza Machi mwakani.