15 Nov 2019 / 46 views
Italia kucheza Bosnia & Herzegovina

Timu ya taifa ya Italy tayari imeshakata tiketi kwenye Kundi J ya kucheza fainali za Euro 2020, ivyo Mancini upo uwezekano wa kupumzisha wachezaji muhimu kwa mechi hii dhidi ya Bosnia & Herzegovina.

Wakati huo huo, Bosnia bado yapo matumaini ya kucheza play-off na kocha Robert Prosinecki ana ubora wa safu ya viungo wengi hivo upo uwezekano wa Bosnia kupata ushindi.

Kiungo wa Juventus Miralem Pjanic bado ndiye mtu muhimu, wakati Amer Gojak (Dinamo Zagreb) ana jicho kali la kupiga pasi za mabao pia ni fundi mzuri wa kuweka mpira kambani.

Umahili wao utakuwa na muhimu katika kumfanya mshambuliaji wa AS Roma Edin Dzeko kuhusika mapema na mara nyingi kupata mipira inayoweza kuleta madhara kwa Italy.

Italy inakosa msukumo na motisha ambayo ingekuwepo ikiwa wangekuwa bado hawajafuzu, inamaanisha kikosi cha Prosinecki kina nafasi ya kupata matokeo mazuri kwenye ardhi ya nyumbani na kutengeneza nafasi ya kucheza play-off au kufuzu kwenye mchezo wa mwisho.