15 Nov 2019 / 35 views
Uingereza wafuzu michuano ya Euro

Uingereza ilisherehekea mchezo wao wa 1,000 kwa mtindo wa aina yake baada ya kuifunga Montenegro 7-0 kwenye mechi ya kufuzu michuano ya kombe la Euro katika uwanja wa Wembley.

Nohodha wa Uingereza, Harry Kane alifunga hat-trick kwenye mechi hiyo huku Alex Oxlade-Chamberlain akifungua bao kwenye mchezo wake wa kwanza baada ya kukosekana kwenye timu hiyo kwa miezi 18 na Marcus Rashford pia alifunga kwenye mechi hiyo.

Uingereza na Chama cha Soka nchini humo walifurahi tukio hilo muhimu, na gwaride la kihistoria kwenye mechi hiyo pia washindi wa Kombe la Dunia la 1966 waliokuwepo kushuhudia mchezo huo.

Baada ya ushindi huo vijana wa Gareth Southgate wamefuzu moja kwa moja kwenye michuano ya Euro mwakani baada ya kuongoza kundi A.

Kwenye mechi hiyo baadhi ya mashabiki wa Uingereza walionekana kumzomea mchezaji wa Liverpool, Joel Gomez wakati anaingia kutokana na mgogoro wake na mshambuliaji wa Manchester City, Rahim Sterling.

Southgate alimuacha Sterling kwenye mechi hiyo kutokana na mzozo huo lakini wawili hao kwasasa wameonekana kumaliza tofauti zao na kuna uwezekano wa Rahim Sterling kurejeshwa kwenye mechi ijayo dhidi ya Kosovo.