08 Nov 2019 / 24 views
Salah afungukia mechi na Man City

Mshambuliaji wa Liverpool, Mo Salah amesema kuwa ni mapema mno kufikiria kushinda taji la ligi Uingereza hata kama Liverpool itawafunga mabingwa watetezi Manchester City.

Timu hizo zitakutana kwenye mechi ya ligi kuu soka nchini Uingereza katika uwanja wa Anfield siku ya Jumapili na kama watashinda Liverpool watashinda watakuwa wanaongoza ligi hiyo kwa alama tisa dhidi yaManchester City.

Kwa upande wa kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp amesema kuwa mechi ya Jumapili dhidi ya Manchester City ni asilimia 100 wanataka kushinda mchezo huo kulingana na umuhimu wake kwenye mbio za taji.

Liverpool inaingia kwenye mchezo huo ambao haujafungwa kwenye ligi msimu huu lakini Salah, ambaye ameshinda Golden Boot katika misimu miwili kati ya minne iliyopita, amefunga mabao matano tu hadi sasa.

"Kwa kusema ukweli sijali ni nini watu wanatarajia kutoka kwangu. Kadiri ninafunga na timu inashinda ni sawa” Alisema Salah

"Sina haja ya kujali kile watu wanatarajia kutoka kwangu. Hiyo inaweza kuweka shinikizo nyingi juu yako na kukufanya utende vibaya kwenye baadhi ya mechi ninazocheza’ Aliongeza Salah.

Liverpool watawakaribisha Manchester City kwenye mechi ya ligi kuu soka nchini Uingereza katika uwanja wa Anfield siku ya Jumapili huku wakiwa na kumbukumbu ya kutopoteza mechi hadi sasa.