08 Nov 2019 / 20 views
Maddison aitwa kikosi cha Uingereza

Kiungo wa Leicester City, James Maddison ameitwa kwenye kikosi cha Uingereza kwa ajili ya mechi za kufuzu michuano ya Euro mwaka 2020.

Beki John Stones, kiungo wa kati wa Liverpool, Alex Oxlade-Chamberlain na winga Callum Hudson-Odoi wa Chelsea nao wameitwa tena kwenye kikosi hicho kuelekea michezo hiyo ya kufuzu.

Uingereza itacheza na Montenegro mnamo Novemba 14 pamoja na Kosovo mnamo 17 Novemba 17 mwaka huu.

Timu hiyo ya Uingereza inayofundishwa na kocha, Gareth Southgate inaongoza kundi A na wanahitaji kushinda mechi moja ili kujihakikishia kufuzu michuano hiyo itakayofanyika mwakani.

Beki wa kati wa Manchester City anachukua nafasi ya beki wa Everton, Michael Keane ambaye ameachwa kwenye kikosi hicho kutokana na majeraha.

Maddison aliwahi kuitwa kwenye kikosi hicho mara tatu lakini hakuwahi kucheza hivyo sasa anaweza kucheza mechi yake ya kwanza akiwa na timu hiyo ya taifa.

Southgate amesema kuwa kama mchezaji wa Uingereza ana nafasi ya kucheza kwenye timu hii kutokana na uwezo wake anaouonesha kwenye timu yake ya Leicester City.

Pia Southgate amemuongeza kiungo wa Aston Villa, Jack Grealish kwenye kikosi hicho ambapo hapo awali hakuwa kuitwa kwenye kikosi hicho.