08 Nov 2019 / 66 views
Bayern Munich wamkataa Wenger

Klabu ya Bayern Munich wamekataa Arsene Wenger kuchukua nafasi ya ukocha wa timu hiyo baada ya kufukuzwa Niko Kovac mwisho wa wiki iliyopita.

Arsene Wenger alikutana na mwenyekiti wa Bayern Munich, Karl-Heinz Rummenigge Jumatano alasiri ili kufanya mazungumzo kuhusu suala la kuchukua nafasi Kovac.

Kovac alifukuzwa kazi mwishoni mwa wiki kufuatia kipigo kutoka kwa Eintracht Frankfurt 5-1 kwenye mechi ya ligi ya Bundersliga na kubakia nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi hiyo.

Msaidizi wa Kovac Hansi Flick amechukua nafasi ya kama kocha wa mpito wakati Bayern wakitafuta kocha wa kudumu ambapo wamesema kuwa kocha watamtangaza kocha huyo ifikapo Novemba 23 mwaka huu.

Bayern Munich wamekataliwa hadharani na bosi wote wa Paris Saint-Germain Thomas Tuchel na Erik Ten wa Ajax, ambapo kocha wa Ajax amesema kuwa atabakia kwa mabingwa wa Uholanzi hadi mwisho wa msimu.