08 Nov 2019 / 21 views
Manchester United yampiga mtu tatu

Kocha wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer amesema kuwa timu yake imeanza kuimarika baada ya kushinda 3-0 dhidi ya Partizani Belgrade kwenye mechi ya Europa ligi.

Mabao ya kipindi cha kwanza kutoka kwa Mason Greenwood na Anthony Martial huku goli la tatu likifungwa na Marcus Rashford baada na kukamilisha ushindi mnono kwenye mechi hiyo ya Europa ligi.

Matokeo hayo yanawafanya Manchester United kuendelea kuongoza kundi L, Katika mechi ijayo ya michuano hiyo Manchester United watakutana AZ Alkmaar mnamo Desemba 12 na kama wakishinda mechi hiyo watafanikiwa kutinga hatua ya 32 ya michuano hiyo.

"Mara nyingi tumekuwa tikifunga bao 1-0 na hatupati la pili lakini kwasasa vijana wangu  wanajifunza kila siku na hii itawapa nguvu kuelekea kwenye mechi ijayo ya ligi kuu dhidi ya Brighton”.

Manchester United ndio timu pekee katika mashindano hayo haijaruhusu goli kwenye michuano hiyo baada ya kucheza mechi nne.

Walikuwa wamefunga mabao mawili katika michezo yao mitatu ya kwanza na kwenye michuano hiyo licha ya kuendelea kuongoza kundi hilo.