08 Nov 2019 / 117 views
Rais wa Uturuki aishtumu UEFA

Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan amesema kuwa Uefa wamefanya vibaya kuichunguza timu ya taifa ya Uturuki baada ya kushangilia kwa kupiga saluti.

Uefa wamefungua mashtaka ya kinidhamu dhidi ya timu ya taifa ya Uturuki mwezi uliopita baada ya wachezaji wake kushangilia kwa kuonyesha saluti kwenye mechi za kufuzu michunao ya Europa ligi ishara iliyoonekana kusapoti jeshi la nchi hiyo nchini Syria.

Erdogan amesema hii ni sehemu ya kampeni pana ya nchi hiyo hivyo wachezaji wa  michezo wa Uturuki zinaunga mkono operesheni hiyo.

"Wadau wa michezo ambao wanawakilisha nchi yetu nje ya nchi wanakumbwa na kampeni nzito tangu kuanza kwa operesheni," Erdogan alisema katika mkutano na waandishi wa habari huko Ankara.

"Tunakataa ubaguzi wa Uefa, tabia isiyo ya haki na kisiasa kuelekea timu yetu ya taifa na vilabu," ameongeza.

Wachezaji hao walifanya salamu za kijeshi wakati wa nyimbo na baada ya mabao dhidi ya Albania na Ufaransa mwezi uliopita.

Mkuu wa opereshenUefa Philip Townsend amesema kuwa timu hiyo inachunguzwa kutokana na kitendo hicho cha kusalimia kijeshi.