08 Nov 2019 / 27 views
Ibrahimovic kurejea AC Milan

Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United, Zlatan Ibrahimović anajiandaa kurudi AC Milan wakati mchezaji huyo atakapoondoka LA Galaxy.

Mshambuliaji Erling Braut Haaland,19, anaweza kujiunga na klabu RB Leipzig akitokea Red Bull Salzburg msimu ujao pamoja na kutolewa macho na Manchester United, Liverpool na Arsenal.

Barcelona imesema ina nia ya kumsajili mshambuliaji wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, 30, kutoka Aresnal itakapofika mwezi Januari.

Manchester United, Tottenham na Wolves wanawania saini ya mshambuliaji James Rodriguez,28, wa Real Madrid mwezi Januari.

Crystal Palace wanafuatilia maendeleo ya mshambualiaji Wout Weghorst,27 ambaye amefunga magoli manane katika michezo 15 akiichezea Wolfsburg.

Arsenal watapambana na West Ham kumsajili mchezaji wa nafasi ya ulinzi Martin Hinteregger, 27, wa Eintracht Frankfurt.

Bournemouth na Wolves wana nia ya kumpata mshambuliaji wa Huddersfield Karlan Grant mwezi Januari.

Bayern Munich haitamteua Arsene Wenger kuwa kocha wake ingawa kocha huyo wa zamani wa Arsenal ameeleza nia yake ya kuwa kocha wa Bayern Munich alipokuwa akizungumza kwa njia ya simu na mwenyekiti wa klabu. Karl-Heinz Rummenigge.

Mkurugenzi wa michezo wa klabu ya Paris St-Germain Leonardo amesema kauli ya kocha wa Real Madrid, Zinedine Zidane kuwa mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ufaransa Kylian Mbappe, 20, kuwa ana ndoto ya kuchezea mabingwa hao wa La Liga ni ya ''kuudhi''.

Mchezaji wa nafasi ya ulizi ya Southampton Cedric Soarea amesema ataondoka kwenye klabu hiyo mwishoni mwa msimu.

Mchezaji wa zamani wa Manchester United na Skauti wa Juventus amesema kuwa kiungo Paul Pogba,26, ataenda kwenye timu ya Italia.

Mchezaji wa nafasi ya ulinzi wa timu ya Arsenal Kieran Tierney, 22, amesema ni juu ya wachezaji wenyewe uwanjani kutatua matatizo ya klabu yanayoendelea.