09 Oct 2019 / 83 views
Mbappe aachwa kikosi cha Ufaransa

Mshambuliaji wa Ufaransa, Kylian Mbappe ameondolewa kwenye kikosi cha Ufaransa kitakachocheza mechi za kufuzu michuano ya Euro 2020 dhidi ya Iceland na Uturuki kutokana na kuwa majeruhi.

Mbappe ambaye amekuwa akipambana na majeraha mara kwa mara nafasi yake imekuchuliwa na mchezaji wa Borussia Moenchengladbach, Alassane Plea.

Ufaransa wamesafiri kwenda Iceland kwa ajili ya mechi hiyo ya kundi H siku ya Ijumaa kabla ya kuwakaribisha Uturuki kwenye Uwanja wa Stade de Ufaransa Jumatatu.

Mabingwa hao wa dunia ni wa pili kwenye Kundi H wakiwa na alama 15, nyuma ya Uturuki wakati Iceland ni ya tatu ikiwa na alama 12 baada ya kucheza mechi sita.

Mechi za kufuzu michuano ya Euro zinaendelea wiki hii katika viwanja tofauti ili kujihakikishia timu hizo zinashiriki michuano ya Mataifa ya Ulaya (Euro) mwakani.