09 Oct 2019 / 25 views
Mourinho kuchukua mikoba ya Pochetino

Kocha wa zamani wa Chelsea na Manchester United, JOSE Mourinho ni Mmoja anayetajwa kwenda kuchukua mikoba ya Mauricio Pochentino kuinoa Tottenham Hotspur.

Mourinho amehusishwa kuchukua mikoba hiyo kutokana na kufanya vibaya kwa timu hiyo msimu huu huku Mourinho akiwa hana timu toka alipofukuzwa kwenye klabu ya Manchester United mwaka jana.

Pochentino yupo kwenye presha kubwa kwa sasa baada ya timu yake kupoteza kwa kipigo cha mabao 7-2 na Bayern Munich kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa nyumbani.

Pia timu yake ilichapwa na timu ya Ligi Daraja la Pili, Colchester United katika michuano ya Carabao Cup.

Kichapo cha mabao hayo 7-2 inaelezwa kuwa ni kikubwa kwa timu hiyo kukipata tangu kuanzishwa kwake miaka 137.

Pochentino amesema kuwa hali wanayopitia kwa sasa ni ya muda tu mambo yatakaa sawa kwenye klabu hiyo hivyo watu wasiongelee vibaya mwenendo wa timu hiyo.

Kutokana na hali hiyo baada ya wadau wa mpira wamesema kuwa kuna uwezekano wa Mourinho kuchukua mikoba ya kocha huyo kutokana na mwenendo mbovu wa timu hiyo msimu huu licha ya kusajili baadhi ya wachezaji.