09 Oct 2019 / 181 views
AC Milan yamfukuza kocha wake

Klabu ya AC Milan umemfuta kazi kocha wake, Marco Giampaolo akiwa na miezi mitatu na nusu tangu apewe mkataba wa kuifundisha timu hiyo.

Kocha huyo ameiongoza Milan kucheza jumla ya mechi saba msimu huu huku akishinda mitatu pekee.

Katika mechi hizo tatu za ushindi, Giampaolo ameiwezesha Milan kujikusanyia jumla ya alama tisa ikiwa kwenye nafasi ya 13 ya msimamo wa ligi.

Giampaolo alichukua mikoba ya aliyekuwa kiungo wa timu hiyo, Gennaro Gattuso mwenzi Juni mwaka huu ambaye aliondoka kufutia kushindwa kuiwezesha timu hiyo kupata nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Milan waliifunga Genoa 2-1 baada ya Pepe Reina kuokoa penati wakati wa dakika za majeruhi lakini walifungwa mechi tatu mfululizo dhidi ya wapinzani wao Inter, Torino na Fiorentina.

Giampaolo aliondoka Sampdoria mwishoni mwa msimu uliopita baada ya kuwaongoza kwenye mchezo wa tisa uliowekwa kwenye Serie A.

AC Milan, mabingwa mara saba wa Ulaya, hawajacheza kwenye Ligi ya Mabingwa tangu 2013-14 na mara ya mwisho walishinda taji la Serie A mnamo 2011.

Klabu hiyo ilifuzu michuano ya Europa ligi mwaka huu lakini ikaondolewa baada ya kuvunja sheria za haki za kifedha na kufungiwa misimu miwili.