09 Oct 2019 / 50 views
Sanamu ya Ibrahimovic yazinduliwa Sweden

Sanamu ya mshambuliaji wa zamani wa Manchester United na timu ya taifa ya Sweden, Zlatan Ibrahimovic limejengwa katika mji wa Malmo nchini Sweden.

Sanamu hilo limetengenezwa kwa muundo wa shaba limewekwa na chama cha soka nchini Sweden lilizinduliwa mbele ya mamia ya mashabiki nje ya uwanja Malmo nchini Sweden siku ya Jumanne.

"Haijalishi unatoka wapi, uko wapi, haijalishi unaonekanaje, sanamu hiyo ni ishara kwamba kitu chochote kinawezekana," alisema Ibrahimovic.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 38 alifunga mabao 62 katika michezo 116 akiwa na timu ya taifa ya Sweden kati ya mwaka 2001 na 2016.

Sanamu hiyo, iliyoundwa na msanii wa Sweden, Peter Linde, ina urefu wa futi 8 na inchi 9 Pia ina uzito karibu kilo 500 baada ya kukamilika kwa sanamu hilo.

Ibrahimovic alianza kucheza soka katika klabu ya Malmo kabla ya kwenda kuchezea Ajax, Juventus, Inter Milan, Barcelona, AC Milan, Paris St-Germain na Mnchester United baadaye akahamia Marekani kucheza katika ligi ya MLS mnamo 2018.

Nahodha wa zamani wa England David Beckham, Ureno na Juventus mbele Cristiano Ronaldo na mshambuliaji wa Liverpool, Mohamed Salah wametengenezewa sanamu kama hilo.