09 Oct 2019 / 15 views
Schweinsteiger atundika daruga

Mchezaji wa zamani wa Bayern Munich, Manchester United na Ujeruamani, Bastian Schweinsteiger ametangaza kustaafu soka akiwa na umri wa miaka 35.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35 alitangaza uamuzi wake siku mbili baada ya kumalizika kwa msimu wa Ligi Kuu ya Soka nchini Marekani akiwa anachezea klabu ya Chicago.

Schweinsteiger alishinda Kombe la Dunia la 2014 na Ujerumani, na pia mataji manane ya Bundesliga akiwa na Bayern Munich huku akicheza jumla ya mechi 121 kwenye timu ya taifa ya Ujerumani toka 2004 hadi 2016.

Kiungo huyo alicheza michezo 500 akiwa na Bayern Munich ambapo pia alishinda Ligi ya Mabingwa Ulaya kabla ya kujiunga na Manchester United kwa Pauni 14.4m mnamo 2015 lakini alishindwa kuzoea Ligi Kuu ya Uingereza.

Schweinsteiger alijiunga na Chicago Fire kwa uhamisho wa bure mnamo Machi 2017 na alifunga kwenye goli la kwenye mechi yake ya kwanza.

Schweinsteiger alicheza katika mashindano makubwa saba mfululizo kwa Ujerumani, akiiongoza timu hiyo kushinda Kombe la Dunia mwaka 20014 huku akishiriki michuano mengine mikubwa  ya Euro 2008 na nusu fainali ya Euro 2012 na 2016.

"Yeye ni mmoja wa wachezaji wakubwa katika historia ya Ujerumani," meneja Joachim Low alisema. "Siku zote tutakuwa na nafasi kwake na upande wa kitaifa. Unaweza kuhisi mapenzi yake kila wakati kushinda. Alikuwa mchezaji mzuri na tabia kubwa."

Mtendaji mkuu wa Bayern Karl-Heinz Rummenigge alisema "milango katika Bayern daima inafunguliwa" kwa mchezaji wao wa zamani.