09 Oct 2019 / 14 views
Bale ataka kuondoka Madrid

Mshambuliaji wa Real Madrid Gareth Bale amechoshwa kuwepo katika klabu hiyo ya Uhispania na badala yake anataka kuondoka.

Bale alitarajiwa kujiunga na klabu ya ligi kuu ya Uchina Jiangsu Suning kwa mkataba wa miaka mitatu majira ya joto akitarajiwa kulipwa £1m kwa wiki lakini Real ilikatiza makubaliano hayo kwasababu waliitisha ada ya uhamisho.

Mnamo Julai, kocha wa Real Madrid, Zinedine Zidane amesema kuwa tunatarajia aondoke hivi karibuni kauli ambayo wakala wa Bale, Jonathan Barnett alijibu kuwa: Zidane hana heshima kwa mchezaji ambaye amejitolea sana kwa Real Madrid.

Bale ameshinda mataji manne ya ubingwa wa Ulaya, taji moja la ligi ya Uhispnania, la Copa del Rey na matatu ya Uefa Super Cups na Club World Cups akiwa Real, na amefunga zaidi ya magoli 100.

Baada ya kutibuka kwa makubaliano ya uhamisho wake kwenda China, mchezaji huyo wa kimataifa wa wales alijitoa katika mechi ya kabla kuanza msimu huko Munich - hatua iliyoelekewa kwamba hayupo sawa kimawazo kuweza kucheza.

Alirudishwa katika timu ya Real msimu huu, na kufunga mechi saba kutokana na kwamba wamesogea juu ya ligi hiyo ya Uhispania La Liga.

Lakini aliachwa nje ya kikosi kilichocheza wiki iliyopita katika mechi ya Champions League dhidi ya Club Bruges, kabla ya kurudi katika kikosi cha kwanza katika mechi waliopata ushindi wa 4-2 dhidi ya Granada Jumamosi.

Bale aliambiwa kuwa Zidane, ambaye amekuwa na uhusiano wa kikazi naye, alifanya uamuzi kuwa anajitayarisha kwa kuondoka kwake.

Wakala wake, Jonathan Barnett, alikwenda kumtafutia nafasi nyingine, lakini Bale alipendelea kusalia katika klabu hiyo.