12 Sep 2019 / 19 views
Wenger: Man Uinted aina uwezo kushinda EPL

Kocha wa zamani wa Arsenal, Arsene Wenger amesema kuwa kikosi cha sasa cha Manchester United hakina uwezo wa kushindana na kutwaa ubingwa wa ligi kuu soka nchini Uingereza msimu huu.

United wameshinda kombe la ligi kuu chini Uingereza mara 20 lakini hawajashinda taji hilo tangu msimu wa mwisho wa Alex Ferguson mnamo 2012-13 hadi leo hawajawahi kushinda kombe hilo.

Wenger amesema kuwa baadhi ya wachezaji wa sasa hawana uwezo wa kuchezea timu hiyo kwasababu hawana vigezo kabisa wa kuwa wachezaji wa Manchester United.

"Unapowaona wanacheza, sio kama timu inayogombea ubingwa kwasababu hawachezi kama walivyokuwa wanacheza kwa kujitoa wachezaji wa zamani kama vile Giggs, Scholes na Beckham” alisema Wenger.

Kwa upande wa mshambuliaji wa zamani Machester United, Andy Cole amesema kuwa mashabiki wa timu hiyo lazima wawe na subira kwani United, ambao walikuwa wa sita msimu uliopita wanafanya kazi ili kufanya timu kuwa bora kama ilivyokuwa zamani.

Cole ambaye alishinda mataji matano ya ligi na ubingwa wa ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 1999 wakati wa miaka yake sita akiwa na Manchester United amesema kuwa anaamini bado wana miaka michache kukaa vizuri.

Cole amesema kuwa Manchester inapaswa kuendelea kuleta wachezaji bora na kujaribu kuboresha timu msimu kwa msimu, kwa sababu timu mbili za juu Liverpool na City zinazofanya vizuri kwasasa nazo zilikuwa kama Manchester City miaka ya nyuma.

Manchester United itacheza na Leicester City kwenye mechi ya ligi kuu soka nchini Uingereza siku ya Jumamosi katika uwanja wa Olt Trafford baada ya kumalizika kwa mechi za kimataifa.