12 Sep 2019 / 1.9k views
Ronaldo aweka rekodi mpya Ulaya

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo ameweka rekodi ya kuwa mchezaji mwenye magoli mengi kwenye mechi za kufuzu michuano ya Euro.

Ilikuwa rekodi nyingine iliyowekwa na Cristiano Ronaldo baada ya kuvunja rekodi iliyowekwa na aliyekuwa mshambuliaji wa Jamhuri ya Ireland, Robbie Keane ambaye alikuwa anashikiria rekodi hiyo.

Ronaldo alifikia rekodi hiyo baada ya kufunga magoli manne kwenye mechi ya kufuzu michuano ya Ulaya dhidi ya Lithunia na kufikisha jumla ya magoli 25 kwenye mechi za kufuzu michuano ya Euro.

Kabla ya mechi hiyo, Keane alimtaka Ronaldo asishinde goli ili aendelee kushikiria rekodi hiyo aliyoudumu nayo kwa miaka mitano.

Kupitia ukura wake wa Instagram Kean alimtania Ronaldo kwa kumuambia kuwa asifunge kwenye mechi hiyo kwasababu alishaweka rekodi nyingi.

Baada ya kushinda magoli hayo manne kwenye mechi hiyo, Ronaldo amezifunga jumla ya timu 150 tofauti kwa vilabu na nchi toka aanze kucheza mpira katika vila mbali mbali barani Ulaya.

Ronaldo sasa amefunga mabao 93 ya kimataifa, 16 nyuma ya anayeshilia rekodi hiyo Duniani, Ali Daei wa Iran pia ni wa kwanza kwa wachezaji wa Ulaya kufunga mabao mengi kwa nchi yake.