12 Sep 2019 / 32 views
Shabiki ajiua nchini Iran

Shabiki wa kike aliye kamatwa akiingia kwenye mechi ya mpira wa miguu Irani, afariki dunia baada ya kujiteketeza kwa moto nchini Iran baada ya kukamatwa uwanji.

Sahar Khodayari binti wa Irani aliyewekwa kizuizini kwa kuvaa kama mwanaume na kwenda kwenye uwanja wa mpira wa miguu kutazama mechi amekufa baada ya kujiwashia moto mara baada ya kubaini anaweza kutumikia jela miezi sita

Kifo cha kuumiza cha Sahar Khodayari mwenye umri wa miaka 29 kimeshika kasi kwenye vyombo vya habari na kwenye mitandao ya kijamii, baadhi ya klabu na wachezaji wamekemea kitendo cha wanawake kuzuiwa kwenda viwanjani kupitia mtandao wa twitter (FC Barcelona,Paul Pogba, As Roma, Gary Lineker)

Tukio ili linakuja pia uku FIFA ikiwa inashirikiana na viongozi wa Iran kuondoa vikwazo vya wanawake kuingia viwanja vya michezo ya wanaume, vikwazo hivyo viliwekwa tangu Mapinduzi ya Kiislam ya nchi hiyo mwaka 1979. FIFA inataka suala hilo kutatuliwa kabla ya Oktoba 10 mwaka huu.

FIFA imekuwa ikijaribu kuishinikiza Iran kuwaruhusu wanawake kuingia kwenye mechi. Mnamo Novemba mwaka jana Iran ilitoa kibali cha muda kwa mamia ya wanawake wa Irani, waliotengwa na mashabiki wa kiume, waliruhusiwa kuingia kwenye Uwanja wa Azadi mjini Tehran kutazama fainali ya Ligi ya Mabingwa Asia.